java

ABOUT US




Establishment and Mandate

UMOJA WA WAJASILIAMALI NA UFUGAJI MWANZA (UWANAUMWA) is the Swahili word which means “The union of Entrepreneurs and Livestock/Pastoralists in Mwanza”. UWANAUMWA is a Non-profit organization founded in 2013 and registered in 2015 with Registration number RE.NO.S.A.20297 as Civil Society Organization (CSO), UWANAUMWA was established to make impact on the growth of entrepreneurs and livestock keepers in Mwanza Tanzania East Africa. UWANAUMWA deals with poultry
and livestock to be precise, ( UWANAUMWA engages with production and raising of hens, cows, goats, pigs, fish, bees and farming activities)

UMOJA WA WAJASILIAMALI NA UFUGAJI MWANZA(UWANAUMWA) 

Goal

  • to promote cooperation  to  all  the  entrepreneurs,  breeders  and  the  to entire population closer to the operations of UWANAUMWA.
  • to improve the lives of orphans and of other people living in vulnerable conditions.
  • responding to community needs  in primary schools, medical,  economic, and victims of various disasters
  • to promote cooperation with governmental and non-governmental organizations to foster development.

Office Location
Visit our head office at
Street Igoma Kati,Igoma Ward, Musoma road. Opp. Olympic Petrol station Block No013/041 SQT. Igoma District Nyamagana Mwanza region TANZANIA EAST AFRICA.
Vision
We envision engaging the community in entrepreneurship and farming activities so that they can meet their basic needs.
Mission
To provide a joint platform for the members of Mwanza to combine the little they have so as they eventually get sound development .
OBJECTIVE
  • Setting up multiple projects
  • Raising capital by all legal available means
  • Cooperating with the government of the United Republic of Tanzania through the local government.

UMOJA WA WAJASILIAMALI NA UFUGAJI MWANZA
(UWANAUMWA)
Umoja wa wajasiliamali na ufugaji Mwanza lengo letu ni kuleta ushirikiano, amani, na mapendo kwa wajasiliamali na wafugaji wote, na jamii nzima ya watanzania. Na kwa kuwa misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika Umoja wenye demokrasia, ambao watendaji wake ni huru, wanaotekeleza wajibu wao bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za kila mwana Umoja zinadumishwa na kulindwa,  na wajibu wa kila mwana Umoja unatekelezwa kwa uaminifu.
Kutokana na hilo ilionekana kuna umuhimu wa kuanzisha Umoja ambao utawaunganisha wajasiliamali na wafugaji wa Mwanza, na Tanzania bara kwa ujumla, ili waweze kuwaelimisha wanachama wake na jamii kwa ujumla kuishi katika hali ya kimaadili na kujishughulisha na kazi  halali za ujasiliamali na ufugaji. Iwapo Umoja kitajiimarisha kiuchumi Umoja utawasaidia watoto yatima, walio katika mazingira magumu, na katika mambo mbalimbali kama elimu, chakula katika shule za msingi, mahitaji ya shuleni, matibabu na pia familia masikini au duni.

wajane, waathirika wa majanga mbalimbali kama UKIMWI,  moto, mafuriko na nk. Chama pia kitakuwa na haki ya kukuza ushirikiano na asasi zisizo za kiserikali na zilizo za kiserikali. za ndani na nje ya nchi.
Ulianzishwa mwaka 2013 ikiwa na wanachama waanzilishi 11

UWANAUMWA. Reg. No.S.A.20297
ilipata usajili wakudumu kutoka serikali kuu mwaka 2015 kama umoja wa wajasiliamali na ufugaji Mwanza {Uwanaumwa}

Makao Makuu ya Ofisi

Makao makuu ya Umoja yatakuwa  Kata ya Igoma mtaa wa Igoma kati, Wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza.


Pia tunaweza kufungua ofisi ndogo za Umoja wetu ndani ya Tanzania bara.


Dira

Kuona wana Umoja wanajishughulisha kwa bidii ili kufikia  malengo yao ya kiuchumi katika shughuli za ujasiliamali na ufugaji kisha kuwasaidia wahitaji wa misaada.


Dhima:

Kutoa huduma bora kwa wananchi na kuboresha maisha ya wanachama wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla.

Malengo ya chama

a)   Kuwawezesha wana Umoja  kimaendeleo na kiuchumi

b)  Kutoa na kupewa semina mbalimbali zinazohusu  kazi zetu za ujasiliamali na ufugaji

c)   Kuanzisha miradi mbalimbali

d)  Kutafuta mitaji kwa kukopa kutoka mabenki ili kuongeza uwezo wa mtaji kwa wanaumoja na wanachama kwa ujumla.

e)   Kushirikiana na serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mamlaka mbalimbali za serikali kama serikali za mitaa, Kata, Wilaya Mkoa na Taifa  kwa ujumla katika kutoa elimu ya ujasiliamali na ufugaji ili watanzania wenzetu wajikwamue kiuchumi  kupitia ujasiliamali na ufugaji.












No comments:

Post a Comment